NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI – JWTZ

Spread the love

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kidato cha nne na kidato cha sita. Aidha, uandikishaji utahusisha vijana waliopo katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ‘Operesheni Jenerali Venance Mabeyo’ na waliomaliza mkataba ambao wamefanya mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na kwa Mkataba wa kujitolea.

Vijana wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

Awe raia wa Tanzania.

Awe na umri usiozidi miaka 25.

Awe na afya nzuri na akili timamu.

Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa.

Awe na cheti halisi cha kuzaliwa.

Awe na vyeti vya shule.

Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha kuzuia Magendo.

Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea miaka miwili (2) au mafunzo ya Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NI IFUATAVYO:-

Kwa vijana waliopo katika makambi ya JKT ‘Operesheni Jenerali Venance Mabeyo’ taratibu zao zinaratibiwa na Makao Makuu ya Jeshi.

Kwa vijana waliopo nje ya Makambi ya JKT, maombi yao yaandikwe kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi, Dodoma kuanzia tarehe 01 Agosti, 2024 hadi tarehe 14 Agosti, 2024 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-

Nakala ya kitambusho cha Taifa au namba ya NIDA.

Nakala ya cheti cha kuzaliwa.

Nakala za vyeti vya Shule.

Nakala ya cheti cha JKT.

Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.

MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO:

Mkuu wa Utumishi Jeshini,

Makao Makuu ya Jeshi,

Sanduku la Posta 194,

DODOMA, Tanzania

Source: https://www.tpdf.mil.tz/news/nafasi-za-kuandikishwa-jeshini

See also: Nafasi ya Kazi EA Foods Ltd – Bajaj Driver