Elon Musk Kutoza $20 Kwa Uthibitishaji wa Twitter – Ripoti. Twitter inatazamiwa kuanza tozo ya huduma yake ya kipekee , kwa kulazimisha akaunti zilizothibitishwa kulipa ada ya $19.99 kila mwezi ili kuendelea kuwa na alama ya uthibitisho kwenye mtandao huo, huku bosi na Mmiliki mpya Elon Musk akithibitisha Jumapili iliyopita kwamba mchakato huo “unafanyiwa kazi”, kulingana na ripoti ya jarida la The Verge.
Twitter Blue – huduma ya hiari ya usajili ya jukwaa kwa vipengele vilivyoongezwa – itapanuliwa ili kujumuisha huduma ya lazima ya uthibitishaji, ripoti hiyo inasema, na kuongeza kuwa watumiaji waliothibitishwa watapewa siku 90 za kulipa au kupoteza hali yao ya kudhibitishwa.
Wakati Huo huo Meneja wa uwekezaji Ross Gerber pia anadai mtendaji mkuu alimweleza kwamba sehemu ya kukaza mkanda wa Musk itajumuisha kupunguzwa kwa 50% kwa wafanyikazi wa Twitter.
Pamoja na mpango huu wa Elon Musk Kutoza $20 Kwa Uthibitishaji wa Twitter – Ripoti , Vile Vile Musk amefuta bodi ya wakurugenzi ya Twitter na kujiteua yeye mwenyewe kuwa mjumbe wake pekee.
Soma pia : Meta yatoa sasisho Jipya liitwalo ‘WhatsApp Community’
Kulingana na kampuni iliyowasilisha faili kwenye Tume ya Usalama na Ubadilishanaji ya Fedha ya Marekani, Bret Taylor, mwenyekiti wa zamani wa bodi hiyo, na Parag Agrawal, mtendaji mkuu wa zamani, ni miongoni mwa wakurugenzi tisa waliofukuzwa kutoka kwenye bodi hiyo ya zamani.